Summary MAELEZO KUHUSU VIAMBISHI MAALUM.
Matumizi ya maneno na viambishi maalum 1. Kwa Hutumiwa ili kuleta au kuonyesha maana zifuatazo: Mahali – ili kuonyesha mahali ni lazima kwa ifuatwe na jina la binadamu. Mf. Tafadhali nionyeshe kwa Namwaya. Hii ni njia ya kwenda kwa mwalimu mkuu. Kesho nitaenda kwa nyanyangu. Umilikaji wa mahali- hupachikwa kwenye mizizi ya viambishi vimilikishi nafsi (-angu, -ako, -enu, -ao) mifano Ninaenda kwao. Unacheza kwako. Analima kwake. Wanalima kwao. Kivumishi cha A- Unganifu kuvumisha nomino za kitenzi jina. Mfano Kucheza kwa Pele kunakumbukwa mpaka leo. Kuimba kwa Mercy Masika kunavutia. Kifananishi. Mfano. Vitu hivyo vinafanana kama shilingi kwa ya pili. Kilinganishi- hasa matokeo katika mashindano fulani. Mfano: Manchester United iliishinda Arsenal mabao nane kwa moja.Kenya Pipeline iliishinda Kenya prisons seti tatu kwa mbili. Pamoja na au jumuiko- kuonyesha mchanganyiko wa vitu au watu. Watu warefu kwa wafuupi wataingia ukumbini. Walikuweko vijana kwa wazee. Alibeba vitabu vyote, vikubwa kwa vidogo. Tulikula chapati kwa mandondo jana. Nilienda katika hoteli hiyo nikaagiza ugali kwa sukuma. Maswali
Written for
- Institution
- KISWAHILI
- Course
- KISWAHILI
Document information
- Uploaded on
- November 28, 2022
- Number of pages
- 16
- Written in
- 2022/2023
- Type
- SUMMARY
Subjects
-
matumizi ya maneno na viambishi maalum 1 kwa hutumiwa ili kuleta au kuonyesha maana zifuatazo mahali – ili kuonyesha mahali ni lazima kwa ifuatwe na jina la binadamu mf tafadhali nionyeshe kwa