NAMBA YAK0…………………………….. SAHIHI ………………….
SHULE………………………………………………………………..
102/2
KISWAHILI
KARATASI YA 2
LUGHA
Saa 2 ½
MTIHANI WA PAMOJA WA HENROK
MUHULA WA TATU – 2022
Maagizo
Andika jina na namba yako katika nafasi ulizoachiwa hapo juu
Jibu maswali yote. Majibu yako yaandikwe katika nafasi zilizoachwa wazi katika
kijitabu hiki cha maswali.
SWALI UPEO ALAMA
1 UFAHAMU 15
2 UFUPISHO 15
3 LUGHA 40
4 ISIMUJAMII 10
JUMLA 80
, 1. UFAHAMU (ALAMA 15)
Soma taarifa hii kisha ujibu maswali yanayofuata.
Ulikuwa wakati wa jioni jua limepunguza udhia wake na upepo mwanana
ulikuwa ukipita na kuzipapasa ngozi zetu mfano wa pamba. Kama ilivyokuwa desturi
yetu hapo kijijini, siku hiyo pia tuliketi nje ya nyumba yetu tukafanya duara kulizunguka
birika la kahawa. Kila mmoja alichukua glasi akajimiminia kiasi cha kahawa alichotaka
na kurudi kuchukua mahali pake kitini.
Tulipotia fahamu tulipata mazoea haya yamekita mizizi nasi tukawa hatuna budi
kuyaakumbatia. Hatukuyakumbatia tu, bali tuliyakumbatia kwa dhati ya moyo. Vikao
hivi havikuwa tu hazina kubwa kwetu bali pia vilikuwa vya thamani isiyomithilika. Hapa
ndipo tulinoleana bongo kwa kupashana habari. Leo hii tumo katika kuzungumzia nguzo
kuu za maendeleo, tena maendeleo ya haja ambayo yataibadilisha sura ya mwananchi nan
chi. Nahodha wa kikao cha leo anampa msemaji wa kwanza nafasi naye hakusita kushika
usukani.
“Nionavyo mimi, maendeleo yatawezekana ikiwa elimu itaweza kukidhi haja za
watu. Sio nadharia tupu ambayo huwezi kuitumikiza ikaleta matokeo. Lazima nchi
imwezeshe kila mtu kupata elimu ya msingi ambayo itamsaidia kufikia habari za
kimsingi, iwe ni kupitaa kwa magazeti au vitabu. Habari hizo zitamfunua macho, akaona
na kuhakiki mambo. Wenzangu, jibu ni elimu! Maendeleo yanategemea elimu,” kijana
mmoja alisema kwa hemko.
Muda wote huo kila mtu alikuwa ametulia. Wapo waliotikisa vichwa kukubaliana
naye na wapo waliovitikisa kukataa. Hata hivyo, walikuwepo waliokaa tu kama mawe.
Hawakuonyesha ishara yoyote ya kuguswa na maneno yale. Mwendesha mjadala alifanya
ishara na mara kijana wa miraba mine aliyekuwa amevaa shati lililompwaya akasimama
na kuzungumza kwa sauti nzito.
“Mtazamo wangu mimi bwana ni tofauti. Ukitazama duniani kote, kila nchi
iliyoendelea imewezekana sana viwandani. Uzalishaji wa viwandani ndio dawa mjarabu.
Hebu vuta fikra1 kila tunachotumia kuanzia kalamu, kitabu, nguo, msumari, saruji …
yaani kila kitu chenye nafasi katika maisha yetu kimepitia hatua za uzalishaji
viwandani…”
“Si ndio hayo! Naona unaniunga mkono aisee! Viwandani huendeshwa kwa elimu
au ukipenda maarifa. Na maarifa hayo huja kwa mafunzo ambayo ni elimu,” alifafanua
yule kijana wa kwanza.
“Nipe muda Sudi! Nipe muda nimalizie hoja yangu. Ninachokisema ni kuwa
elimu bila utumizi wake kuzalisha huduma na bidhaa muhimu haina nafasi kubwa katika
maendeleo ya jamii. Elimu inafaa kuzalisha. Na uzalishaji muhimu Zaidi ni wa
2|Page